15 Desemba 2020 - 13:15
Rais Rouhani: Iran iko tayari kuipatia Uganda uzoefu wake wa kielimu na kiufundi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kuipatia Uganda uzoefu wake wa kielimu na kiufundi katika nyanja mbalimbali.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo wakati alipopoteka hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Uganda, Bw. Muhammad Tezikuba Kisambira na kusema kuwa, uhusiano wa Tehran na Kampala ni wa kiurafiki kwa miaka mingi. Amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapenda kustawisha uhusiano wake na Uganda katika nyuga zote.

Aidha Rais Rouhani amejibu ombi la balozi huyo kuhusu kushiriki zaidi mashirika ya Iran katika kuhamishia nchini Uganda teknolojilia na elimu za kisasa kwa kusema, serikali yake itazidi kuyahamasisha mashirika ya Iran hasa yanayojihusisha na masuala ya viwanda, elimu na teknolojia kushiriki zaidi katika miradi ya ujenzi na miundombinu ya Uganda.

Vile vile amegusia mwaliko wa Rais wa Uganda wa kumtaka afanye ziara rasmi nchini humo na kuelezea matumaini yake kwamba ziara hiyo itafanyika katika muda unaofaa.

Kwenye mazungumzo hayo, Balozi Muhammad Tezikuba Kisambira wa Uganda hapa Tehran, mbali na kukabidhi hati zake za utambulisho amesema kuwa, nchi yake inapenda kufaidika vizuri na maendeleo makubwa ya kielimu na kiufundi ya Jamhuri ya Kiislamu na ameyataka mashirika ya Iran yashiriki zaidi katika miradi ya maendeleo ya Uganda na yawapatie wananchi wa nchi hiyo uzoefu wao katika mambo tofauti.

Vile vile amemkabidhi Rais Hassan Rouhani, mwaliko rasmi wa Rais Yoweri Kaguda Museveni wa Uganda wa kumwalika kufanya ziara rasmi nchini humo.

342/